Sura Al-Humazah

سُورَةُ الهُمَزَةِ

Makkiya · aya 9 · Juzuu 30

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

Hifadhi Sura Al-HumazahSoma kwa sauti na Shamsa inasikiliza, ikikuonyesha neno uliloruka au ulilokosea. Pamoja na matamshi ya Kilatini, bure.

Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani

وَيْلٌۭ لِّكُلِّ هُمَزَةٍۢ لُّمَزَةٍ ﴿١﴾

1. Ole wake kila safihi, msengenyaji!

ٱلَّذِى جَمَعَ مَالًۭا وَعَدَّدَهُۥ ﴿٢﴾

2. Aliye kusanya mali na kuyahisabu.

يَحْسَبُ أَنَّ مَالَهُۥٓ أَخْلَدَهُۥ ﴿٣﴾

3. Anadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele!

كَلَّا ۖ لَيُنۢبَذَنَّ فِى ٱلْحُطَمَةِ ﴿٤﴾

4. Hasha! Atavurumishwa katika H'ut'ama.

وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا ٱلْحُطَمَةُ ﴿٥﴾

5. Na nani atakujuvya ni nini H'ut'ama?

نَارُ ٱللَّهِ ٱلْمُوقَدَةُ ﴿٦﴾

6. Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa.

ٱلَّتِى تَطَّلِعُ عَلَى ٱلْأَفْـِٔدَةِ ﴿٧﴾

7. Ambao unapanda nyoyoni.

إِنَّهَا عَلَيْهِم مُّؤْصَدَةٌۭ ﴿٨﴾

8. Hakika huo utafungiwa nao

فِى عَمَدٍۢ مُّمَدَّدَةٍۭ ﴿٩﴾

9. Kwenye nguzo zilio nyooshwa.

Tafsiri © Ali Muhsin Al-Barwani. Maandishi ya Kiarabu (Uthmani): Mradi wa Tanzil.

Katika programu ya Shamsa unaweza kusikiliza kila sura, kuweka alama ulipoishia na kusoma bila intaneti.