Sura Al-Fil

سُورَةُ الفِيلِ

Makkiya · aya 5 · Juzuu 30

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

Hifadhi Sura Al-FilSoma kwa sauti na Shamsa inasikiliza, ikikuonyesha neno uliloruka au ulilokosea. Pamoja na matamshi ya Kilatini, bure.

Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani

أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِأَصْحَٰبِ ٱلْفِيلِ ﴿١﴾

1. Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo?

أَلَمْ يَجْعَلْ كَيْدَهُمْ فِى تَضْلِيلٍۢ ﴿٢﴾

2. Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika?

وَأَرْسَلَ عَلَيْهِمْ طَيْرًا أَبَابِيلَ ﴿٣﴾

3. Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi,

تَرْمِيهِم بِحِجَارَةٍۢ مِّن سِجِّيلٍۢ ﴿٤﴾

4. Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni,

فَجَعَلَهُمْ كَعَصْفٍۢ مَّأْكُولٍۭ ﴿٥﴾

5. Akawafanya kama majani yaliyo liwa!

Tafsiri © Ali Muhsin Al-Barwani. Maandishi ya Kiarabu (Uthmani): Mradi wa Tanzil.

Katika programu ya Shamsa unaweza kusikiliza kila sura, kuweka alama ulipoishia na kusoma bila intaneti.