Dua Kutoka Qur'ani
Dua kutoka Qur'ani kwa Kiarabu cha msahafu. Tafsiri ni ya Ali Muhsin Al-Barwani; sura na aya zimeandikwa chini ya kila dua.
Mema ya dunia na Akhera
رَبَّنَآ ءَاتِنَا فِى ٱلدُّنْيَا حَسَنَةًۭ وَفِى ٱلْءَاخِرَةِ حَسَنَةًۭ وَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ ﴿٢٠١﴾
Rabbana atina fid-dunya hasanatan wa fil-akhirati hasanatan wa qina 'adhaban-nar
Mola wetu Mlezi, tupe duniani mema, na Akhera mema, na utulinde na adhabu ya Moto!
Dua aliyokuwa akiiomba Mtume ﷺ mara nyingi zaidi; katika riwaya hiyo inaanza kwa "Allahumma" (Bukhari 6389).
Qur'ani, Al-Baqarah 2:201 · Bukhari 6389 · Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani
Usituchukulie hatiani
رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَآ إِن نَّسِينَآ أَوْ أَخْطَأْنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَآ إِصْرًۭا كَمَا حَمَلْتَهُۥ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِۦ ۖ وَٱعْفُ عَنَّا وَٱغْفِرْ لَنَا وَٱرْحَمْنَآ ۚ أَنتَ مَوْلَىٰنَا فَٱنصُرْنَا عَلَى ٱلْقَوْمِ ٱلْكَٰفِرِينَ ﴿٢٨٦﴾
Rabbana la tu'akhidhna in nasina aw akhta'na, rabbana wa la tahmil 'alayna isran kama hamaltahu 'alalladhina min qablina, rabbana wa la tuhammilna ma la taqata lana bih, wa'fu 'anna waghfir lana warhamna, anta mawlana fansurna 'alal-qawmil-kafirin
Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama ulio wabebesha wale walio kuwa kabla yetu. Mola wetu Mlezi Usitutwike tusiyo yaweza, na utusamehe, na utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde kaumu ya makafiri.
Qur'ani, Al-Baqarah 2:286 · Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani
Zithibitishe nyoyo zetu
رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً ۚ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْوَهَّابُ ﴿٨﴾
Rabbana la tuzigh qulubana ba'da idh hadaytana wa hab lana min ladunka rahmah, innaka antal-Wahhab
Mola wetu Mlezi! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kwisha tuongoa, na utupe rehema itokayo kwako. Hakika Wewe ndiye Mpaji.
Qur'ani, Ali 'Imran 3:8 · Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani
Dua ya Adam na Hawa
رَبَّنَا ظَلَمْنَآ أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلْخَٰسِرِينَ ﴿٢٣﴾
Rabbana zalamna anfusana wa in lam taghfir lana wa tarhamna lanakunanna minal-khasirin
Mola wetu Mlezi! tumejidhulumu nafsi zetu, na kama hutusamehe na kuturehemu, hakika tutakuwa katika wenye kukhasirika.
Waliisema Adam na Hawa baada ya kuteleza kwao, wakiomba msamaha.
Qur'ani, Al-A'raf 7:23 · Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani
Nijaalie nidumishe Swala
رَبِّ ٱجْعَلْنِى مُقِيمَ ٱلصَّلَوٰةِ وَمِن ذُرِّيَّتِى ۚ رَبَّنَا وَتَقَبَّلْ دُعَآءِ ﴿٤٠﴾ رَبَّنَا ٱغْفِرْ لِى وَلِوَٰلِدَىَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ ٱلْحِسَابُ ﴿٤١﴾
Rabbij-'alni muqimas-salati wa min dhurriyyati, rabbana wa taqabbal du'a'. Rabbanaghfir li wa li-walidayya wa lil-mu'minina yawma yaqumul-hisab
Mola wangu Mlezi! Nijaalie niwe mwenye kushika Sala, na katika dhuriya zangu pia. Ewe Mola wetu Mlezi, na ipokee dua yangu. Mola wetu! Unighufirie mimi na wazazi wangu wote wawili, na Waumini, siku ya kusimama hisabu.
Dua ya Ibrahim. Aya yake ya pili husomwa mara nyingi katika kikao cha mwisho cha Swala.
Qur'ani, Ibrahim 14:40-41 · Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani
Kwa ajili ya wazazi
رَبِّ ٱرْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِى صَغِيرًۭا ﴿٢٤﴾
Rabbir-hamhuma kama rabbayani saghira
Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni.
Qur'ani, Al-Isra 17:24 · Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani
Nikunjulie kifua changu
رَبِّ ٱشْرَحْ لِى صَدْرِى ﴿٢٥﴾ وَيَسِّرْ لِىٓ أَمْرِى ﴿٢٦﴾ وَٱحْلُلْ عُقْدَةًۭ مِّن لِّسَانِى ﴿٢٧﴾ يَفْقَهُوا۟ قَوْلِى ﴿٢٨﴾
Rabbish-rah li sadri, wa yassir li amri, wahlul 'uqdatan min lisani, yafqahu qawli
Ewe Mola wangu Mlezi! Nikunjulie kifua changu, Na unifanyie nyepesi kazi yangu, Na ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu, Wapate kufahamu maneno yangu.
Dua ya Musa kabla ya kuanza utume wake; mara nyingi husomwa kabla ya kusoma au kuzungumza.
Qur'ani, Ta-Ha 20:25-28 · Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani
Nizidishie elimu
رَبِّ زِدْنِى عِلْمًۭا ﴿١١٤﴾
Rabbi zidni 'ilma
Mola wangu Mlezi! Nizidishie ilimu.
Qur'ani, Ta-Ha 20:114 · Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani
Dua ya Yunus
لَآ إِلَٰهَ إِلَّآ أَنتَ سُبْحَٰنَكَ إِنِّى كُنتُ مِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ ﴿٨٧﴾
La ilaha illa anta subhanaka inni kuntu minaz-zalimin
Hapana mungu isipo kuwa Wewe Subhanaka Uliye takasika. Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu.
Aliiomba Yunus akiwa tumboni mwa samaki mkubwa. Hakuna Muislamu anayeomba kwayo kwa jambo lolote isipokuwa Mwenyezi Mungu humjibu (Tirmidhi 3505).
Qur'ani, Al-Anbiya 21:87 · Tirmidhi 3505 · Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani
Dua ya Ayyub
أَنِّى مَسَّنِىَ ٱلضُّرُّ وَأَنتَ أَرْحَمُ ٱلرَّٰحِمِينَ ﴿٨٣﴾
Anni massaniyad-durru wa anta arhamur-rahimin
Mimi yamenipata madhara. Na Wewe ndiye unaye rehemu kuliko wote wanao rehemu.
Aliisema Ayyub katika ugonjwa wake wa muda mrefu.
Qur'ani, Al-Anbiya 21:83 · Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani
Mwenyezi Mungu anatutosha
حَسْبُنَا ٱللَّهُ وَنِعْمَ ٱلْوَكِيلُ ﴿١٧٣﴾
Hasbunallahu wa ni'mal-wakil
Mwenyezi Mungu anatutosha, naye ni mbora wa kutegemewa.
Aliisema Ibrahim alipotupwa motoni, na Mtume ﷺ alipoambiwa kwamba jeshi limekusanyika dhidi yake (Bukhari 4563).
Qur'ani, Ali 'Imran 3:173 · Bukhari 4563 · Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani
Mimi ni mhitaji wa kheri yoyote
رَبِّ إِنِّى لِمَآ أَنزَلْتَ إِلَىَّ مِنْ خَيْرٍۢ فَقِيرٌۭ ﴿٢٤﴾
Rabbi inni lima anzalta ilayya min khayrin faqir
Mola wangu Mlezi! Hakika mimi ni mhitaji wa kheri utakayo niteremshia.
Aliisema Musa huko Madyan, akiwa mgeni asiye na kitu.
Qur'ani, Al-Qasas 28:24 · Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani
Samehe na urehemu
رَبِّ ٱغْفِرْ وَٱرْحَمْ وَأَنتَ خَيْرُ ٱلرَّٰحِمِينَ ﴿١١٨﴾
Rabbighfir warham wa anta khayrur-rahimin
Mola wangu Mlezi! Samehe na urehemu nawe ni Mbora wa wanao rehemu.
Qur'ani, Al-Mu'minun 23:118 · Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani
Kwa ajili ya mke, mume na watoto
رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَٰجِنَا وَذُرِّيَّٰتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍۢ وَٱجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا ﴿٧٤﴾
Rabbana hab lana min azwajina wa dhurriyyatina qurrata a'yunin waj'alna lil-muttaqina imama
Mola wetu Mlezi! Tupe katika wake zetu na wenetu yaburudishayo macho, na utujaalie tuwe waongozi kwa wachamngu.
Qur'ani, Al-Furqan 25:74 · Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani
Kwa ajili ya waliotutangulia
رَبَّنَا ٱغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَٰنِنَا ٱلَّذِينَ سَبَقُونَا بِٱلْإِيمَٰنِ وَلَا تَجْعَلْ فِى قُلُوبِنَا غِلًّۭا لِّلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ رَبَّنَآ إِنَّكَ رَءُوفٌۭ رَّحِيمٌ ﴿١٠﴾
Rabbanaghfir lana wa li-ikhwaninalladhina sabaquna bil-iman, wa la taj'al fi qulubina ghillan lilladhina amanu, rabbana innaka Ra'ufun Rahim
Mola wetu Mlezi! Tughufirie sisi na ndugu zetu walio tutangulia kwa Imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walio amini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu.
Qur'ani, Al-Hashr 59:10 · Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani